![]() |
Mario Balotelli |
Mchezaji mtukutu kutoka AC Milan anatarajiwa kujiunga na
timu ya Liverpool muda wowote baada ya ada ya uhamisho Pauni 16 milioni
kukubaliwa.
Hata hivyo swala ambalo analiogopa kocha wa Liverpool Brendan
Rodgers ni mwenendo wa tabia ya mchezaji huyo anapokuwa nje au ndani ya
uwanja.
Balotelli amekuwa mchezaji mwenye vituko sana na jazba, na hapendi
kuonewa.
Vikwazo vilivyokuwepo kwa sasa ni makubaliano ya
kimkataba ambayo
yatamuhusu yeye Balotelli na myenendo yake kitabia. Hilo likifikwa muafaka basi
dakika yoyote, atatua Anfield. Kinachotia matumaini ni
mchezaji huyo tayari amewaaga wachezaji wenzake kwamba anaiacha club yao muda
wowote kuanzia sasa, na ameshawaaga hata wafanyakazi wengine.
0 comments:
Post a Comment