Smart life inakupa habari motomoto
kwa nini 95% ya vijana kwa masikitiko makubwa wanajikuta wanaisha kuwa marafiki na si wapenzi.
Smart life wanasema kuondokona
na hali hiyo ya kutoka kwenye urafiki wakudumu (friend zone) ni moja ya maswali
mengi wanayopata kuulizwa kila siku.
smart life wanasema, Kuna
sababu kuu mbili ambazo zinakukwamisha kila siku kushindwa kutoka katika "Friend
zone”
1. Uwoga wa kutokuwa karibu.
Wadau
wengi wa design hii hujikuta wapo karibu lakini siku zote wanaishi na
kuheshimiana kama kaka na dada. Huenda kila mmoja akiwa na matumaini ipo siku
mambo yatakuwa mazuri. Sijui kila mtu anadhani kuna mmoja ataamka asubuhi na
kumwambia mwenzie “hey naomba tuwe wapenzi” kisha uruke kwa furaha? Mhhhh Laa hasha
mambo hayapo hivyo.
Kinacho
kulazimu kufanya ni kuweka mazingira
yanayowavuta au kuleta hisia ya mapenzi kati yenu, kama kukumbatiana mnapokuana tightly, kushikana mikono mnapotembea na kushika bega au shingo kwa sekunde kadhaa wakati wa maongezi yakila siku. Lakini taratibu na si kwa kasi ya ajabu kama vile unamshika mtu ambaye tayari ni mpenzi wako. Chakufanya unafanya kwa style ya kuibiaibia, acha uwoga Kama unataka kutoka kwenye “friend zone” lakini hili halikufikishi unapotaka kufika, ila litakusaidia.
2. Kuleta hamasa baada ya mvuto.
kama
nilivyosema kuna njia chache sana za kuweza kutoka kwenye “friend zone”, kuna
kitu muhimu ningependa kuwapa tahadhari mapema. Kuna mbinu yakizamani ambayo
haitakusaidia sanasana itakupotezea muda, mbinu hizo ni kama vile kuomba kutoka
out kupata drinks au dinner, hayo tupilia mbali kabisa. Niyakawaida sana na
hayana msukumo wowote labda kama mlishapendana basi mnatafuta sababu za kushawishiana.
Kuna
njia mpya ambazo zita leta msisimko kwako na kwa mrembo pia ambazo zitakuletea
ushindi mapema.
Kwanza
kabisa omba mkutane sehemu tulivu yenye mvuto na itakayo mfanya ajisikie vizuri
na awe na confidence yakutosha. Kuna vigezo vichache ambavyo mkiwa hapo
vinaweza kuleta msisimko na muwashawasha Zaidi kwa wote wawili.
Hata
kama umekutana na warembo ambao hawakuwa na shauku au hawana time na wewe basi
utaona matokeo yake mazuri na ushirikiano toka kwao.mualike mrembo eneo lile
lile mlilo kutana mwanzo ilia pate confidence.
Nini
chakufanya kwanza.
Ukiwa
katika eneo hilo jaribu kuongea na watu wa jirani wakike na kiume na
usimkodolee mrembo wako macho muda wote mkiwa hapo. Hii itakusaidia kwani
itamfanya awe attracted kwako. Pale akiona kama wanawake wengine wanamsukumo au
furaha ya uwepo wako basi itamfanya mrembo azidi kuchanganyikiwa kutaka kuwa
karibu na wewe Zaidi, hii itamfanya nae afanye vitu ambavyo vitakupa attention
kwake. Hapo ndo patamu sasa!
Hiyo
ndo itakuwa ndi golden chance yakuweza kukupa ushindi yakujitawwala na kudodosa
machache wakati mkipiga story ndogo ndogo zinazoendana na mazingira, zingatia
kuwa hiyo sio siku yaw ewe kurefusha mazungumzo marefu bali ni kuleta hamasa,
ushawishi na kuweka mazingira mpaka pale atakapo kuwa kwenye himaya yako siku
zijazo na kujichukulia ushindi.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjxWX1qtKBQ6g1eBocwpbe5LYFSCcT7Ww6l4MDZYT1xuyUq-dXG-3dtlNSS7Fa9od6MhJVON4YX98DtFBB2Ar51ub2x6OPOvVBR4bmHbMYefOpmvLNy0bFLVFuZq_cWATiHqisghxbVTqM/s1600/images+(6).jpg)
Ongeza
hali ya ukaribu na mgusano ambao unamfanya ajisike raha na kutojua hata
chakufanya na kukuacha ufanye unachotaka wewe. Kibaya Zaidi wanaume wengi
hawafikii hiyo level yenye amasa na mvuto kwa warembo kuwa tayari kwa mahitaji
ya wanaume na yao kiujumla. Try first to reach a peak!!
0 comments:
Post a Comment