Menu

Sami Khedira kuktua Arsenal 
Imethibitika Sami Khedira kakubali kutua Arsenal, habari zinazo toka kwa Guillem Balague kwamba Chelsea wamesita mojo kwa moja kuweka nguvu za kutosha kwa kiungo mkabaji wa Real Madrid Sami Khedira kwani wameshahisi kuna makubaliano binafsi yameshafanyika ili kuweza kumchukua mchezaji huyo ambaye dau lake limeshuka hadi Pauni 12 kutoka pauni 27. Kuporomoka huko kwa bei ya mchezaji huyo ni kukubali kumuuza kwa shingo upande ili kutopata hasara mwakani kwani ataondoka free of charge. Kwahiyo sasa imebaki kazi kwa Arsenal kumwaga mapesa yamnyakue mchezaji huyo ambae kwasasa inathibitika kila kitu kipo shwari.

Hata hivyo kocha wa Chelsea Jose hajatia nguvu ya kutosha licha kuwa na ukaribu au nafasi kubwa ya kuweza kuchukua mchezaji kwa kuwa ana wachezaji viungo wakutosha kama Nemanja Matic, John Mikel Obi, Cesc Fabregas and the Brazilian Ramirez. 
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

0 comments:

Post a Comment

 
Top