Menu

Arsenal wapata fursa ya kuweza kumsajili  Marco Reus  kama Borussia Dortmund wataridhia baada ya mchezaji wao kugoma kusaini mkataba mpya, Reus ambaye katosa mkataba mpya na Dortmund.
kocha wa Arsenal-Arsene Wenger mbioni kumsajili Marco Reus
Mapema mwezi huu, Marco ameleta vita kwa timu za Ulaya lakini Gunners imeripotiwa kwa kuongoza mbio hizo za kumsaka mchezaji huyo matata akiwa uwanjani. 
Inasemekana kutokana na kuongezeka kwa majadiliano kwamba Reus anaweza kuuzwa msimu huu majira ya joto,  Mkurugenzi Mtendaji Hans-Joachim Watzke wa Dortmund amekataa mchezaji huyo kuuzwa na kudai kuwa swala kubwa si pesa, tutatizama namna gani ya kumbakiza mchezaji wetu. 'Sisi tusubiri na kuona kama tunaweza kuongeza umiliki wa Marco,' alisema Watzke.
Marco Reus amabaye garama yake itashuka hadi pauni 19.8milioni majira ya pili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, msimu ujao itakuwa ngumu sana kumbakiza katika kikosi chao na hivyo wanaweza kulzimika kumuuza kipindi hiki ili kukwepa hasara.
hata hivyo Atletico Madrid na Manchester United walikuwa mbioni kusaka saini ya mchezaji huyo lakini jitihada za kibiashara haikufanyika.

0 comments:

Post a Comment

 
Top