Hivi Manchester united wanatumia mbinu za kisiasa kucheza mpira?
Nilikuwa najiuliza hilo swali lakini baadae nikapata majibu
yakutosha.
Najua unafahamu Manchester United chimbuko lake wapi! Ni Uingereza,
hivi huwa unaona jinsi uingereza (England) ikiwa inajiandaa kama vile kombe la
Dunia? Kuna timu itakayoonyesha mbwembwe kama uingereza kabla hata mashindano
hayajaanza? Magazeti yataandika habari hata ambazo zikisema Rooney alikuwa
anakula apple kabla ya mazoezi, au mchezaji Fulani maarufu eti kaenda kununua
perfume Fulani supermarket kabla ya mechi!, habari ambazo hata uwanjani hazitahitajika. Basi tu ndo walivyo na mbwembwe zao kuonekana wenyewe ndo wanajua starehe kuliko wengine
ulimwenguni. Unakumbuka ile habari yao iliyosema wachezaji wao wameruhusiwa
kwenda na wake zao? sisi inatuhusu nini? wachache wameoa pale, ila walimaanisha waende na wachumba zao
wakale bata. Mbwembwe nje ya uwanja nyingi kuliko uwanjani. na hatimaye hutolewa mapemaa na kubaki kula bata kama ambavyo wamezoea, Nijibu tu umewahi kusikia
udaku wowote kwa timu ngangari kama Ujerumani? Wanaoona kazi hata kuongea na
waandishi wa habari, pia huonyesha furaha kwa hisia pale wanapofanikiwa baada
ya ushindi!
Kuna swali jepesi tu jamaa mmoja ameuliza Man united ni
mashetani walio potea au ni masimba dume walio lala?
wameanza msimu huu kwa mbwembwe huku wakishinda mechi za kjipima kama dume la simba, lakini kwenye ligue kilaiini wanafungika. walisema timu ipo imara sana, sasa hivi nasikia wanasema timu itachukua hata miezi 3 kuwa fiti, si unakumbuka yale ya Moyes?
Mbona timu yenye pesa zakutosha na wachezaji maradufu kama
Manchester City hatuwasikiki kwenye vyombo vya habari na udaku kama Man United utafikiri hawana walezi. Utafananisha
kiwango cha mmoja mmoja na wachezaji wa Man City? Majibu ni City watashinda
kabla hata yakuingia uwanjani.
Ohh! Wananifanya nianze kuifananisha na timu ya Yanga nchini Tanzania
ambayo inashangilia mapema na kuwapa kipaumbele wachezaji wa nje ambao hata hawajawahi kuwaona
wakicheza uwanjani, chaajabu ndio wanao pewa sifa na huduma nzuri kulioko hata wengine
muhimu ambao wengi wao ni wazawa.
0 comments:
Post a Comment